DeroscUliza WhatsAppZangu

Msaada, sheria na marejesho

Duka hili linaendeshwa na Derosc · +255 629 888 978

Sheria

  1. Unaponunua filamu au sehemu za mfululizo kwenye Derosc, unapata haki ya kuitazama hapa na kuipakua kwa matumizi yako binafsi. Hairuhusiwi kuisambaza, kuiuza tena au kuionyesha hadharani.
  2. Malipo ni ya mara moja kwa kila filamu au kundi la sehemu. Bei inaonyeshwa kabla hujalipa, na ndiyo bei pekee utakayolipa.
  3. Kutazama hakuna kikomo: filamu uliyolipia unaweza kuitazama hapa wakati wowote kwa link yako au kwa namba yako ya simu kupitia “Zangu”.
  4. Kupakua kuna kikomo cha majaribio 3 kwa kila sehemu — kundi la sehemu 6 lina majaribio 18. Hakuna muda wa mwisho. Ukifika kikomo bado unaweza kutazama.
  5. Link yako ni yako. Ukiipa mtu mwingine, majaribio yake ya kupakua yanahesabiwa kwako.

Marejesho

  1. Marejesho yanatolewa pale tu huduma haikupatikana kabisa: umelipa na filamu haichezi wala haipakuliwi, au mfumo wote ulikuwa umezimika wakati huo. Hapo unarudishiwa pesa zako zote.
  2. Ukilipa mara mbili kwa bahati mbaya kwa kitu kile kile, malipo ya ziada yanarudishwa.
  3. Filamu inayocheza vizuri haina marejesho — si kwa ladha, si kwa kubadili mawazo. Trela na maelezo yapo ili uamue kabla ya kulipa.
  4. Kudai: tuma ujumbe hapa chini na namba uliyolipia, au wasiliana kwa +255 629 888 978. Tutathibitisha tatizo na kurudisha pesa kwa namba ile ile uliyolipia.

Maoni

Kuna tatizo, au unataka kitu? Mwambie duka. Namba ya simu inawaruhusu kukujibu.